VOLUME 1, ISSUE 1

Mada: Dhamira za Maradhi, Uganga na Tiba za Asili katika Fasihi Simulizi


Mwandishi: Gerephace Mwangosi

 Chuo Kikuu Katoliki Ruaha, S.L.P 774, Iringa, Tanzania.

Correspondence: mwangosigerephace@yahoo.com


Ikisiri


Makala haya yameangazia dhamira za uganga, maradhi na tiba za asili katika jamii ya Wanyakyusa. Hoja kuu ilikuwa ni kwamba dhamira hizo zimekuwa na usawili hasi katika nyimbo za Magosi za jamii teule. Ili kuijadili hoja hii, data za msingi za makala haya zilikusanywa mkoani Mbeya katika halmashauri ya Busokelo kwa kurejelea nyimbo za Magosi za jamii ya Wanyakyusa. Data za msingi zilikusanywa kwa mbinu za mahojiano na majadiliano. Uchambuzi na mjadala wa data zilizowasilishwa katika makala haya uliongozwa na nadharia ya Usosholojia. Miongoni mwa matokeo ya makala haya ni kuwa jamii haziwezi kustawi katika harakati za maendeleo yake kama zitaendelea kukumbatia imani za uchawi na ushirikina. Kushamiri kwa imani hizo kunasababisha pia kupuuza jitihada za kisayansi na kisasa za namna bora na sahihi za kupambana na UKIMWI. Aidha, waganga wa tiba za kijadi hawana budi kufanya kazi zao kwa weledi, uaminifu na uadilifu kwa kuzingatia misingi bora ya maarifa na utamaduni uliosheheni masuala yenye tija kwa manufaa ya ustawi wa jamii. Makala haya yanahitimisha kuwa ushauri wa kitaalamu na kiwakati unapaswa kufanyika katika jamii zote hapa nchini ili kukabiliana na maradhi, pamoja na imani za uchawi na ushirikina zilizoshamiri na kuleta maafa katika jamii. Kwa ujumla, haipendezi katika karne hii ya 21 kuamini kuwa nguvu yoyote tusiyoijua ina maana ya ushirikina na uchawi.

Maneno Msingi: Maradhi; Uganga; Tiba za Asili; Nyimbo za Magosi; Jamii ya Wanyakyusa


Download the Article